Skip to main content
Skip to main content

Sherehe za mahari zageuka maombolezo baada ya ajali

  • | Citizen TV
    13,397 views
    Duration: 3:08
    Sherehe za mahari zimegeuka kilio na majonzi baada ya watu saba kufariki katika ajali ya barabarani kilomita mbili kabla ya kufika nyumbani kwa wakwe zao. Familia katika eneo la Kalembwani, Kibwezi, Kaunti ya Makueni, imeachwa katika maombolezo kufuatia mkasa huo, huku watu wengine 60 wakijeruhiwa. Saba hao walifariki baada ya matatu waliyokuwa wakisafiria kuanguka bondeni baada ya dereva kushindwa kulidhibiti.