Sheria ya fedha ya 2023 itaendelea kutumika hadi mahakama ya juu itakapotoa uamuzi wake

  • | K24 Video
    4 views

    Sheria ya fedha ya 2023 itaendelea kutumika hadi mahakama ya juu itakapotoa uamuzi wake kuhusu rufaa iliyowasilishwa na waziri wa hazina ya kitaifa. Ikitoa agizo hilo, mahakama ya kuu ilizingatia kutokuwa na uhakika kuhusu hatua za kukusanya mapato na ugumu ambao unaweza kujitokeza katika uendeshaji wa mihimili ya serikali. Uamuzi wa rufaa hiyo umepangwa kufanyika mwezi septemba na hadi wakati huo, kodi zilizowekwa chini ya sheria hiyo zitaendelea kukusanywa .