Shirika la 'Future Health Africa' latoa matibabu ya bure ya mifupa kwa wakaazi wa Laikipia

  • | Citizen TV
    126 views

    Wakazi wa Kaunti ya Laikipia watanufaika na matibabu ya bure ya mifupa kwa muda wa wiki mbili. Matibabau hayo yanatolewa na shirika la Future Health Africa kwa ushirikiano na hospitali ya rufaa ya Nanyuki. Matibabu haya yanalenga kuwafanyia upasuaji baadhi ya wagonjwa mia mbili hamsini wenye matatizo ya viungo na mifupa na kuwachunguza wagonjwa wengine 2,500 ambao wana shida mbalimbali za mifupa. kulingana na gavana wa kaunti ya Laikipia Joshua Irungu, kambi hiyo ya matibabu pia itawafaa wagonjwa kutoka kaunti jirani za Meru, Nyandarua, Isiolo, Samburu na Nyeri.