Shirika la KWS latakiwa kuchukua hatua zaidi kuhusu ndovu kaunti ya Kwale

  • | Citizen TV
    160 views

    Kaunti ya Kwale inaitaka idara ya huduma za wanyama pori kuchukua tahadhari za dharura ili kuwazuia wanyamapori kuvamia mashamba ya wakazi na kuharibu mimea. Wakizungumza katika kongamano la wasimamizi wa shirika la msalaba mwekundu kutoka kaunti 47, naibu gavana wa kaunti hiyo Chirema Kombo na mshrikishi wa shirika hilo ukanda wa Pwani Hassan Musa, wamesema ndovu wameanza kuvamia baadhi ya mashamba katika maeneo ya Lungalunga na Kinango ambako mimea inaanza kunawiri. Viongozi hao Wamesema hali hiyo itaregesha nyuma hatua zilizopigwa kukabili kiangazi na kusababisha njaa na hivyo kuitaka huduma kwa wanyamapori KWS kujukumika.