Shirika la Msalaba Mwekundu litaruhusiwa kuwatembelea mateka waliosalia huko Gaza.

  • | VOA Swahili
    476 views
    Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema wakati wa kikao fupi mnamo Jumatano (Novemba 22) Shirika la Msalaba Mwekundu litaruhusiwa kuwatembelea mateka waliosalia huko Gaza. Israel na Hamas walikubaliana Jumatano kusitisha mapigano huko Gaza kwa angalau siku nne, kuruhusu misaada na kuwaachilia mateka wasiopungua 50 wanaoshikiliwa na wanamgambo katika eneo la Palestina badala ya Wapalestina 150 waliofungwa jela nchini Israel.