- 106 viewsDuration: 1:27Wakaazi zaidi ya elfu mia moja kutoka eneo pana la Magharibi katika kaunti za Kakamega, Bungoma, Vihiga na Busia watanufaika na nguvu za umeme kutoka shirika la uzambazaji umeme mashinani REREC . Kulingana na mkurugenzi mtendaji wa REREC daktari Rose Mkalama, mpango huo utagharimu shilingi bilioni sita nukta tatu kwa kusambaza nguvu za umeme katika baadhi ya shule na hata masoko. Wenyeji wakishabikia mpango huo wakisema utaboresha biashara zao na kuwezesha kujikimu kimaisha.