Kituo cha ndondi chazinduliwa

  • | Citizen TV
    282 views

    Kama njia ya kuukuza mchezo wa ndondi nchini, shirika la Ultra Fight Series limezindua kituo cha kuutangaza mchezo huo. Kulingana na washikadau wa mchezo huo nchini, ni sharti mchezo huo uendeshwe kisasa ili Kenya kurudi kutamba tena kwenye ulingo wa ndondi sawa na mashabiki kurudi kuupenda tena. Wanalenga kuandaa mapigano manne makuu kwa mwaka yatakayohusisha wanandondi tajika nchini, afrika na duniani kote.