Shughuli ya ukaguzi wa DNA zatarajiwa kuanza ili kutambua miili ya walioaga dunia Endarasha

  • | Citizen TV
    2,991 views

    Shughuli ya ukaguzi wa chembe chembe za msimbojeni wa DNA zinatarajiwa kuanza hii leo ili kutambua miili ya wanafunzi walioaga dunia katika mkasa wa moto shuleni Hillside Endarasha kaunti ya Nyeri. Watoto 21 walipoteza maisha yao katika mkasa huo huku kufikia sasa hatma ya wanafunzi 17 ikiwa bado haijulikani. Tuungane naye mwanahabari wetu Kamau Mwangi ambaye yuko katika hospitali ya Naormoru Level 4 kwa maelezo zaidi..