Shughuli za kawaida zatatizika kwa muda eneo la Esoit

  • | Citizen TV
    502 views

    Shughuli za kawaida zilitatizika kwa mara nyingine eneo la Esoit, Transmara baada ya mamia ya wakaazi kujitokeza kulalamikia madai ya unyakuzi wa ardhi eneo hilo. Waandamanaji hao ambao kwa mara ya kwanza walijitokeza wakiwa na hati miliki ya mashamba yao kwa kauli moja wanataka idara ya usalama kuingilia kati utata wa ardhi hiyo kati ya wenyeji na halmashauri ya majani chai nchini KTDA