Shughuli za kutafuta miili kwenye mkasa wa boti kuzama katika mto Tana zinaendelea

  • | Citizen TV
    24,765 views

    Katika kaunti ya Tana River, Shughuli za kuwatafuta waathiriwa wa mkasa wa boti ya jana jioni zimeendelea. Ripoti zikituarifu kuwa watu 23 wanatafutwa. Haya yakiendelea huku waliookolewa wakiendelea kupokea matibabu katika hospitali moja Madogo. Waliozungumza wakisimulia yaliyojiri, wakiwalaumu wasimamizi wa boti hiyo kwa kubeba abiria wengi kupita kiasi.Kwa mujibu wa polisi eneo la Madogo, Kufikia sasa ni watu 20 pekee ambao wameokolewa. Shughuli za kutafuta miili ya wanaoshukiwa kuangamia kwenye mkasa huo zinatarajiwa kuendelea hii leo baada ya kusitishwa jana usiku kutokana na giza. Naibu Gavana wa kaunti hiyo Mahat Ali Loka amesema maafisa wa kaunti hiyo wataanza kusafirisha watu kwa kutumia boti za kaunti