Shughuli za kutengeneza maboti zanoga Pwani

  • | K24 Video
    105 views

    Mabadiliko ya tabia nchi, pamoja na ukosefu wa vifaa muhimu vya uvuvi, imeathiri pakubwa sekta ya uvuvi pwani ya Kenya, iliyo na uwezo wa kiuchumi wa shilingi billioni 300 kila mwaka. Aidha kulingana na taasisi ya utafiti wa masuala ya uvuvi na bahari (KMFRI) hali hiyo huenda ikabadilika, kufuatia mradi wa uchumi wa samawati unaotekelezwa na serikali ya kenya kwa ufadhili wa benki ya dunia, kwa gharama ya shilingi milioni 190 huko Kilifi.