Shule 66 za Nyamira kupokea ufadhili wa shilingi bilioni 1.5 kutoka kwa serikali ya Kuwait

  • | Citizen TV
    295 views

    Shule 66 katika kaunti ya Nyamira zinatarajiwa kupokea ufadhili wa jumla ya shilingi bilioni 1.5 kutoka kwa serikali ya Kuwait ili kuimarisha miundo msingi katika shule hizo. Akizungumza katika shule za upili za Nyambaria na Tombe katika kaunti ya Nyamira, waziri wa elimu Ezekiel Machogu amedokeza kuwa wizara hiyo chini ya uongozi wake Rais William Ruto walizungumza na balozi wa taifa hilo humu nchini na kuwashawishi kuwapa ufadhili huo ili kupiga jeki sekta ya elimu Nyamira. Aidha, waziri wa teknolojia na mawasiliano Eliud Owalo amesisitiza umuhimu wa wananchi, haswa wanafunzi kujifunza kutumia mtandao ili kunufaika na ajira za mtandaoni.