Shule ya Ngoto, Makueni yafungwa

  • | KBC Video
    47 views

    Takriban wanafunzi-1,500 wa shule ya upili ya wavulana ya Ngoto eneo la Nzaui kaunti ya Makueni wameagizwa kwenda nyumbani baada ya kuteketeza bweni.Wanafunzi hao waliokuwa na hamaki walizua vurugu kulalamikia usimamizi mbaya, ukosefu wa maji safi, chakula na uvamizi wa kunguni. Waliteketeza bweni hilo ambalo wanafunzi-175 hulala. Hakuna chochote kilichookolewa kutoka bweni hilo. Hii ni mara ya pili kwa kisa cha moto kutokea shuleni humo mwaka huu. Juhudi za kuzungumza na usimamizi wa shule hiyo ziliambulia patupu.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive