Shule za upili zatakiwa kuwateuwa wanachama wa bodi walio karibu na shule

  • | Citizen TV
    220 views

    Shule za Upili nchini zimetakiwa kuhakikisha zinaweka wasimamizi wa bodi za shule hizo wanachama wanaotoka maeneo yaliyo karibu ili kupunguza gharama za usafiri . Akizungumza katika hafla ya siku ya elimu katika shule ya msingi ya chepsaita, kaunti ndogo ya Turbo huko Uasin Gishu, msaidizi wa rais Farouk Kibet anasema shule zinatumia pesa nyingi kuwalipa wasimamizi wa bodi za shule kwa gharama ya usafiri na marupurupu ya vikao, fedha ambazo zingesaidia kuimarisha miundo msingi shuleni. waziri wa elimu ezekiel machogu ameeleza kuwa serikali inaendelea kuongeza muindomsingi shuleni na kuajiri walimu zaidi ili kuinua viwango vya elimu kote nchini.