- 94 viewsMamlaka ya usambazaji maji ya pwani imekana madai ya magavana wa eneo hilo kuwa wamezembea katika utendakazi wake na kusababisha uhaba wa maji kwa wakazi wa pwani. Afisa mkuu wa mamlaka hiyo hamoud mguza badal yake akisema, mzigo wa madeni ya kaunti umezidi kulemaza kazi zao. Mamlaka hiyo sasa inawataka magavana wa Mombasa, kwale, Kilifi na Taita Taveta kulipa madeni yao ua zaidi ya bilioni moja.