Sifuna:Niko tayari kujiondoa ODM iwapo chama kitamuunga mkono rais Ruto 2027

  • | Citizen TV
    11,122 views

    Katibu Mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna sasa anasema yuko tayari kujiondoa kutoka chama hicho endapo kitakubali kuunga mkono kuchaguliwa tena kwa Rais William Ruto kama Rais kwenye uchaguzi mkuu ujao. Aidha ni msimamo ambao pia umetolewa na mbunge wa Saboti Caleb Amisi wakisema kuwa kamwe hawako tayari kumuidhinisha rais Ruto kuwania urais mwaka wa 2027. Walikuwa wakizungumza eneo la Saboti kaunti ya Trans Nzoia wakati wa hafla ya kuwawezesha kina mama wafanyabiashara