Simba na Yanga nani kusonga mbele Klabu Bingwa Afrika

  • | BBC Swahili
    968 views
    Leo na kesho moto utawaka katika nyasi za uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam Tanzania ambapo kuna michezo miwili ya klabu bingwa Afrika. Leo Simba itaingia dimbani saa tatu usiku kumenyana na Al Ahly kutoka Misri, na kesho Yanga itaumana na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini saa tatu usiku saa za Afrika Mashariki. Ipi nafasi ya timu hizi mbili ambazo zimeweka historia msimu huu kutoka nchi moja kufuzu hatua ya robo fainali na kuingia nusu fainali? Mwandishi wa BBC David Nkya amemzungumza na mchambuzi wa michezo Irene Kilango. #bbcswahili #tanzania #simbanayanga Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw