Simba yaleyale ya 1993, RS Berkane bingwa Shirikisho Afrika

  • | BBC Swahili
    4,944 views
    #bbcswahili #simba #soka #kandanda Tanzania itabidi kuendelea kuwa na subira kabla ya kupata taji la kwanza Afrika kwa ngazi ya klabu, baada ya Simba kukubali kutoka sare ya 1-1 na kufanya matokeo ya jumla kuwa magoli 3-1 dhidi ya RS Berkane ya Morocco iliyoshinda mchezo wa kwanza 2-0. Sasa Berkane ndiyo mabingwa wapya wa kombe la shirikisho Afrka. Matumaini ya mashabiki wa Simba na watanzania yalikuwa makubwa kwa kuzingatia matokeo ambayo Simba imekuwa ikiyapata katika miaka ya karibuni inapocheza nyumbani ukiwepo msimu huu ambao Simba imeshinda michezo yoto ya nyumbani isipokuwa mchezo wa fainali. Matokeo hayo yametonesha Donda la mwaka 1993 Simba ilipofungwa nyumbani 2-0 na Stella Abidjan ya Ivory Coast jijini Dar es Salaam. Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw