Soko la Suq Mugdi Garissa lateketea moto

  • | Citizen TV
    346 views

    Watu watano wamejeruhiwa kufuatia mkasa wa moto katika soko moja la kibiashara mjini Garissa mapema leo Mamia ya wafanyabiashara wanakadiria hasara kufuatia moto huo ulioteketeza majumba ya biashara katika soko la suq mugdi mjini humo. Serikali ya kaunti na wakaazi walishirikiana kuuzima moto huo uliosambaa kwa kasi. Waliojeruhiwa wanapokea matibabu katika hospitali ya rufaa ya garissa. Tukio kama hili pia limeshuhudiwa mjini hola kaunti jirani ya tana river baada ya moto kuteketeza jumba moja la burudani. Moto huu ulisababishwa na hitilafu ya nguvu za umeme.