Somalia yaanza Ramadhan katika kipindi kirefu cha ukame kihistoria

  • | VOA Swahili
    52 views
    Mwezi mtukufu wa Ramadhan Mwaka 2023 umeambatana na kipindi kirefu cha ukame katika historia ya Somalia. Ramadhan imeleta ongezeko la bei za vyakula kwa nchi ambayo tayari inahangaika na mfumuko wa bei uliosababishwa kwa kiasi fulani na uvamizi wa Russia huko Ukraine na mavuno kidogo yaliyosababishwa na miaka mitano ya mfululizo wa misimu ya ukosefu wa mvua. Mamilioni ya mifugo ambayo ndiyo kiini cha lishe kwa watu imekufa, na takriban watu 43,000 kufariki mwaka jana pekee. #somalia #drought #climatechange #ramadan - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.