Spika Amason Kingi atangaza kubanduliwa kwa Gavana Kawira Mwangaza

  • | K24 Video
    32 views

    Spika wa seneti Amason Kingi hii leo ametangaza kubanduliwa kwa gavana wa Meru Kawira Mwangaza afisini katika gazeti rasmi la serikali. hii ni licha ya mahakama kuu kusitisha kutekelezwa kwa uamuzi wa seneti na kumwagiza spika asitangaze nafasi katika afisi ya gavana hadi kesi aliyowasilisha mahakamani itakapoamuliwa. Alipojitetea mbele ya seneti usiku wa kuamkia leo, mwangaza alidai kuwa seneta wa meru kathuri murungi ndiye chanzo cha masaibu yake.