- 1,058 viewsDuration: 1:20Spika wa bunge la Garissa Idle Gure amelazimika kuahirisha vikao na mikutano ya kamati za bunge hilo mara kadhaa kutokana na ukosefu wa idadi inayohitajika ya wakilishi wadi inayoruhusu vikao kuendelea. Hali hii imechangia kuchelewa kwa mijadala na kupitishwa kwa miswada muhimu katika bunge hilo, hali ambayo imechangia kurundika kwa miswada ambayo haijashughulikiwa huku muda wa wakilishi wadi hao ofisini ukizidi kuyoyoma. Spika Gure anasema kuwa wawakilishi wadi wanatelekeza majukumu yao ya uwakilishi na kuwanyima wapiga kura haki yao.