- 919 viewsDuration: 1:40Spika wa Bunge la kaunti ya Isiolo Mohammed Roba ameitaka serikali kuwajibika zaidi katika kesi iliyomhusisha gavana wa kaunti hiyo Abdi Guyo ambapo anadaiwa kupanga njama ya kumteka nyara na kumjeruhi aliyekua Afisa mkuu wa Afya katika kaunti hiyo. Spika Roba akiongea katika eneo la Garsen kaunti ya Tana river ameikashifu idara husika kwa upepetevu akisema kuwa wiki moja baada ya mkurugenzi wa mashataka ya umma kuamuru kukamatwa kwa gavana huyo wa isiolo, amri hiyo haijatekelezwa. Kwa sasa spika huyo amemtaka rais William Ruto kuingilia kati huku akihoji kuwa Abdirahman Hassan Kama muathiriwa amebaki bado hajapata Haki yake. Watu Wengine saba zaidi walitakiwa kukamatwa.