Starlets tayari kuivaa Ethiopia

  • | Citizen TV
    337 views

    Timu ya taifa ya wasichana chini ya miaka 17 imefanya mazoezi yake ya mwisho hii leo uwanjani Ulinzi Complex, tayari kuivaa ethiopia hapo kesho kwenye mechi ya kuwania kufuzu kombe la dunia. Starlets itahitaji ushindi wa aina yoyote kufuzu raundi ya nne na ya mwisho kuelekea kombe la dunia baada ya kukabwa sare tasa ugenini addis ababa wiki jana. Mshindi wa mechi hiyo ya kesho saa tisa mchana atachuana na burundi iliyowanyeshea Djibouti jumla ya mabao 18 kwa bila.