- 602 viewsDuration: 1:16Jamhuri ya Sudan imetangaza kwamba kufikia sasa watu 2,500 wameuwawa katika mji wa El Fashir eneo la Darfur. Naibu balozi wa nchi hiyo Muhammad Akasha Osman amesema kwamba huenda idadi hiyo ikaongezeka kutokana na taharuki inayoendelea tangu kundi la Rappid Support Forces -RSF kuteka mji huo. Osman alihimiza umoja wa mataifa na muungano wa Afrika kuingilia kati na kutuma wanajeshi ili kurejesha amani nchini humo.