SUPKEM inawataka wanasiasa kutoingilia IEBC

  • | Citizen TV
    133 views

    Baraza kuu la waislamu nchini SUPKEM sasa linawataka wanasiasa kukoma kuingilia mchakato wa kuwatafuta makamishna wapya wa tume ya uchaguzi nchini IEBC. Mwenyekiti wa SUPKEM Hassan Ole Naado amesema kuwa yeyote aliye na shaka kuhusu majina yaliyowasilishwa bungeni na Rais William Ruto kuandikia bunge malalamishi hayo kulingana na katiba. Bunge limetangaza kuwa litaandaa usaili wa makamishna wote saba tarehe 26 mwezi huu.