- 1,373 viewsDuration: 5:03Susan Akuya ameishi bila uwezo wa kuona tangu alipokuwa na umri wa miaka kumi. Hali hii hata hivyo haikumvunja moyo binti huyu wa miaka 25 ambaye ni hivi majuzi tu ambapo alifuzu chuo kikuu. Susan alikuwa miongoni mwa maafala zaidi ya elfu waliofuzu kutoka chuo kikuu cha Egerton huko Njoro na kupata shahada ya Utafiti wa Jinsia na Maendeleo. Leo hii tunamvisha taji la mwanamke bomba Susan Akuya aliyefuzu kwa alama ya juu