Taasisi ya 360 Climate yazindua siku ya talanta kwa vijana

  • | Citizen TV
    321 views

    Taasisi ya 360 Climate inayolenga kuwezesha vijana kukuza vipaji iliyoko katika kaunti ya muranga imezindua siku ya talanta ili kuwatafuta vijana wenye vipawa mbalimbali. Aidha vijana kote nchini wamehimizwa kujiunga na kozi za ufundi kama njia ya kujijengea mustakabali mzuri wa kujitegemea. Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya 360 climate, daniel thiong'o, akizungumza katika hafla hiyo ya kutafuta vipaji ambapo wanafunzi na waliohitimu walionyesha ujuzi wao katika kozi mbalimbali, alisema kuwa chuo hicho kinatoa mafunzo ya kiufundi kama njia ya kuwawezesha vijana kujiajiri.