Tabasamu kwa wale wote walioathirika na mbolea feki ya bei nafuu.

  • | West TV
    26 views
    Baada ya vilio na lalama kutoka kwa wakulima mbalimbali kupewa mbolea feki ya bei nafuu, sasa seriikali mejitokeza tayari kuwafidia wakulima walioathirika na mbolea hiyo waliyopokea kupitia maghala ya halmashauri ya nafaka na mazao nchini NCPB. Akihutubia wanahabari katika makao makuu ya wizara ya kilimo baada ya kuwa na mkutano na viongozi wa vitengo husika katika sekta hiyo kama vile NCPB, kephis na KEBS, katibu katika wizara ya kilimo Dkt Paul Ronoh alisema kuwa wizara imeamrisha halmashauri ya NCPB kuwapatia wakulima walioathirika mbolea nyingine mbadala ya kupanda kwa wale ambao hawajapanda na kuwapa mbolea ya kunyunyizia kwa wale ambao tayari wameshapanda.