Takriban raia 52 wameuawa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwezi huu

  • | BBC Swahili
    497 views
    Waasi wanaoungwa mkono na ISIS wameua takriban raia 52 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwezi huu pekee. Mauaji haya yanatokea wakati ambapo waasi wa M23 na serikali ya Rais Felix Tshisekedi wameshindwa kufikia muafaka wa makubaliano ya amani ya Doha, Qatar. M23 wamesema hawatarejea katika mazungumzo ya amani huko Qatar wakidai kanuni za kumaliza vita hazijazingatiwa kikamilifu na serikali ya DRC. Hii inamaanisha nini kwa amani na usalama mashariki mwa Congo? @RoncliffeOdit anaangazia hilo kwa kina katika Dira ya Dunia TV kwenye ukurasa wetu wa YouTube BBC Swahili. #bbcswahili #DRC #M23 Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw