Tanzania Yamkaribisha Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris

  • | VOA Swahili
    243 views
    Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris atajitokeza katika mstari wa mbele wa mapambano ya demokrasia Afrika siku ya Alhamisi, akiwa nchini Tanzania wakati nchi hiyo ikipiga hatua katika kurejesha sifa yake kama serikali yenye kujumuisha watu mbalimbali kitaifa. Samia Suluhu Hassan, rais wa kwanza mwanamke Tanzania, ameondoa baadhi ya sera kandamizi, kama vile kupiga marufuku mikutano ya upinzani, licha ya kuwa aliingia madarakani kama mwanachama wa chama tawala. Harris, mwanamke wa kwanza kuhudumu nafasi ya makamu wa rais wa Marekani, atakutana na Samia Alhamisi, ikiwa ni ishara muhimu ya kuungwa mkono na Washington wakati Marekani ikiimarisha ushirikiano wake na Afrika. #tanzania #samiasuluhuhassan #kamalaharris - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.