Taswira la eneo la Shakahola wanapoangamia wafuasi wa Paul Mackenzie

  • | West TV
    15,136 views
    Baada ya kufunga Kanisa lake la Good News International hapo Malindi na kituo chake cha televisheni cha Times Tv kufungwa, Pasta Paul Mackenzie alibuni mbinu fiche ya kuwavutia wafuasi na kuwafunza imani na itikadi kali ambazo zinaaminika kuenda kinyume na maandiko matakatifu ya Bibilia. Mwanahabari wetu leonard wamalwa alizuru eneo la Shakahola katika kaunti ya Kilifi na kutuletea taswira ya matukio yanavyoendelea katika eneo hilo.