- 7,491 viewsDuration: 47sWizara ya Mambo ya Nje ya Azerbaijan imesema kuwa ndege isiyo na rubani ya Iran imegonga jengo la abiria katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nakhchivan huku ndege nyingine isiyo na rubani ikianguka karibu na jengo la shule eneo la Shakarabad. Maafisa wa eneo hilo wanasema watu wanne wamejeruhiwa. Uwanja huo wa ndege wa kiraia kambi ya kijeshi ya la anga la Azerbaijan zipo katika eneo linalojitawala la Nakhchivan, lililozungukwa na mipaka ya Iran na Armenia. Iran imekanusha kuhusika na shambulio hilo, lakini Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev ameishutumu Iran kwa ugaidi na kuahidi kulipiza kisasi, kwa mujibu wa shirika la habari la Agence France-Presse. #bbcswahilii #iran #wanajeshi Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw