Tembo waangamiza watu wanne Lungalunga, Kwale

  • | Citizen TV
    753 views

    Wakaazi wa vijiji 21 eneo bunge la LungaLunga kaunti ya Kwale wanaishi kwa hofu baada ya ndovu kuvamia vijiji hivyo na kuwauwa watu wanne pamoja na kuharibu mazao yao mashambani. Ndovu hao wanaaminika kutoka katika mbuga ya Tsavo na taifa jirani la Tanzania. Shirika la Huduma kwa wanyama pori nchini KWS limetakiwa kuwajibika na kuhakiksha wanyama hao wamerejeshwa porini ili kuzuia maafa zaidi. Vijiji vilivyoadhirika ni pamoja na Kwanyanje, Mambambarani, Pehoni, Masinga na Mandawacho miongoni mwa vingine.