Tishio la Ebola | Serikali yatakiwa kuimarisha uangalizi

  • | KBC Video
    58 views

    Chama cha matabibu humu nchini kinaitaka serikali kuimarisha uchunguzi kwenye vituo vya mpaka baina ya Kenya na Uganda na pia barabara kuu inayoelekea magharibi mwa Kenya ili kupunguza uwezekano wa chamko la Ebola humu nchini. Maafisa wa chama hicho wakiongozwa na mwenyekiti wao Peterson Wachira na katibu mkuu George Gibora waliibua wasiwasi kuhusiana na kujiandaa kwa nchi hii na pia kaunti zinazochukuliwa kuwa hatarini za maeneo ya magharibi. Viongozi hao walikuwa wakizungumza wakati wa kukagua hali ya kujiandaa kwa kaunti kukabiliana na ugonjwa huo.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1news Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #ebola #News