Tishio linalokabili juhudi za upanzi wa miti nchini

  • | K24 Video
    170 views

    Kenya iko mbioni kupanda miti ili kuongeza kiwango cha miti na misitu, katika juhudi za kuzuia madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi. Aidha juhudi za upanzi wa miti huenda zikahujumiwa na aina moja ya kwekwe ijulikanayo kama ‘dodder,’ ambayo inavamia miti na kuikausha. Dodder ni mmea ambao hauna mizizi wala rangi ya kijani. Kufikia sasa, mmea huo umevamia miti na mimea mingine katika kaunti 12, hali ambayo inahatarisha kapu la chakula endapo hatua za haraka hazitachukuliwa kudhibiti hali..