TSC inakabiliwa na tuhuma za upendeleo

  • | Citizen TV
    601 views

    Kamati ya Bunge kuhusu Elimu hii leo imeishtumu Tume ya kuwaajiri waalimu nchini ya TSC kwa kukiuka masharti ya kamati hiyo hususan kudinda kutoa maelezo kuhusu taratibu za kupandishwa vyeo kwa waalimu 25,000. Wanachama Wa Kamati hiyo wanailaumu TSC kwa kukosa kueleza kinaga ubaga taratibu za kuwapandisha vyeo waalimu huku wakidai kumekuwa na upendeleo.