Tuhuma anazorushiwa mjane anapojaribu kudai urithi wa mumewe

  • | VOA Swahili
    266 views
    Tanzania: Mwanamke aliyefiwa na mumewe na anajukumu la ulezi wa watoto watatu na akiwa mjamzito anaeleza ukandamizaji unaoendelea dhidi ya wanawake katika jamii. Ni kama ilivyo kwa wanawake wengine wanaofikwa na janga la kudhulumiwa urithi hakuambulia chochote katika urithi wa mumewe. Anaeleza tuhuma anazoelekezewa mwanamke wakati anapotaka kufuatilia haki zake, na hivyo kumfanya asiweze kuchukua hatua yoyote. Ungana na mwandishi wetu wa Dar es Salaam Idd Uwesu akifanya mahojiano maalum na mwanamama huyu na kueleza yaliyomfika na mengi mengineyo.. - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.