'Tulikuwa tunaimba ilitusahau shida tulikumbana nazo katika safari yetu kwenda ulaya'

  • | BBC Swahili
    Yankuba ni kijana wa Gambia ambaye alitoroka ukandamizaji na kuanza safari ya kutisha baharini na ardhini kwenda Ulaya. Alipofika Napoli Italia, aligundua mazingira magumu ya ubaguzi wa rangi mbali na idara ya uhamiaji isiopendelea wahamiaji. Alilazimika kutoroka na kujificha katika klabu moja ya burudani katika mji unaoitwa Teranga. Klabu hiyo inatoa fursa isio ya kawaida kwa wahamiaji kucheza densi na kuimba ili kukabiliana na maumivu ya safari yao ya kuelekea Ulaya mbali na ubaguzi wa rangi wanaokabiliana nao chini Itali. #BBCAfricaEye #Uhamiaji #Italia #Ubaguziwarangi