Tume ya EACC yachunguza ubadhirifu wa pesa katika kaunti

  • | Citizen TV
    965 views

    Tume ya kupambana na ufisadi nchini imebaini ubadhirifu wa fedha katika kaunti ya Siaya kufuatia miundombinu hafifu ya kuzuia ufisadi. Katika ripoti iliyowasilshwa kwa gavana wa kaunti hiyo James Orengo, EACC ilitoa mapendekezo mbalimbali ili kuzuia ufujaji wa fedha za umma. Haya yanajiri huku tume hiyo pia ikiitaka bunge la kaunti ya Elgyo Marakwet kutoa maelezo kamili kuhusu malipo ya shilingi milioni 21 kwa wawakilishi wadi katika kaunti hiyo.