Tume ya haki za binaadam yatoa ripoti kwamba kaunti 20 zina idadi kubwa ya mimba za mapema

  • | Citizen TV
    285 views

    Tume ya kutetea haki za kibinadamu imeorodhesha kaunti 20 kama ambazo zina idadi kubwa zaidi ya watoto waliopachikwa mimba nchini. Kaunti ya Nairobi inaongoza kwa visa 452 ikifuatwa na Kakamega kwa visa 328, Bungoma visa 294, Nakuru visa 283 na Kiambu ikifunga orodha ya kaunti tano zilizoathirika zaidi kwa visa 267. kaunti zingine zilizo na idadi kubwa ya mimba za utotoni Kilifi, Meru, Kisii, Machakos na Narok. umaskini, dhuluma za kijinsia, kutokuwepo kwa mafunzo kuhusu mahusiano na mila potovu zimetajwa kama vichocheo vya hali hiyo.