Tume ya SRC yadai madaktari walihadaiwa kusaini mkataba wa maelewano usiowezakutekelezwa

  • | KBC Video
    34 views

    Tume ya kuratibu viwango vya mishahara na marupurupu ya watumishi wa umma-SRC inadai kuwa madaktari walihadaiwa na utawala uliopita kusaini mkataba wa maelewano ambao hautekelezeki. Mwenyekiti wa tume hiyo ya SRC, Lyn Mengich amesema ingawa matakwa ya madaktari ni halali, mkataba wa maelewano wa mwaka-2017 hauwezi kutekelezwa na hivyo madaktari wanapasa kurejelea mazungumzo ili kuafikiana kuhusu matakwa yao. Wito wa Mengich umejiri huku waziri wa utumishi wa umma, Moses Kuria akisema ananuia kuwianisha mikataba yote ya maelewano ya vyama vya wafanyikazi ili kuepusha kuvurugwa kwa huduma zinazotolewa kwa wananchi.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News