Tundu Lissu azungumzia hali yake ya kiafya miaka mitano tangu kushambuliwa

  • | BBC Swahili
    4,923 views
    Miaka mitano kamili iliyopita mwanasiasa wa Tanzania Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana. Lissu kutoka chama kikuu cha upinzani, Chadema alisafirishwa hadi nairobi kwa matibabu na hatimaye kwenda Ubelgiji kwa matibabu zaidi. Bwana Lissu alirejea Tanzania mwaka 2020 na kuwania urais ambapo alishindwa dhidi ya Hayati John Magufuli aliyekuwa akiwania muhula wake wa pili kupitia chama tawala cha CCM. Rais Magufuli alifariki dunia mwaka 2021 na nafasi yake kuchukuliwa na makamu wake, Samia Suluhu Hassan. Bwana Lissu amekuwa akisita kurejea Tanzania kwa madai kuwa na wasiwasi na usalama wake. #bbcswahili #tanzania #siasa