- 286 viewsDuration: 3:24Mabadiliko ya hali ya hewa barani Afrika yamewafanya wabunifu kuongeza juhudi za kutafuta suluhu kwa changamoto zinazoikabili sekta ya kilimo. Katika Mkutano wa Uwekezaji kwenye Mbinu za Kilimo Kinachostahimili Mabadiliko ya Hali ya Hewa, wafadhili na wadau walijadili mikakati mbalimbali, ikiwemo usimamizi wa taka za kikaboni na mbinu za kisasa za uzalishaji wa kahawa. Denis Otieno anaangazia ubunifu huo katika makala ya leo ya Kilimo Biashara.