Uchaguzi Uganda 2021: Bobi Wine asema Waganda wana fursa ya mwisho kuleta mabadiliko

  • | BBC Swahili
    Kampeini za uchaguzi mkuu nchini Uganda zinakamilika rasmi leo licha ya kuwa baadhi ya wagombea wa kiti cha urais tayari wamekamilisha mikutano yao ya kampeini. Mgombea wa upinzani wa chama cha National Unity Party NUP Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine amelalamika kuwa kampeini zake zimevurugwa kiasi kikubwa na utawala wa sasa. Mwandishi wetu Roncliffe Odit alizungumza naye na kwanza anaanza kwa kumueleza jinsi kampeini zake zilivyokuwa. #bbcswahili #uchaguziuganda2021 #uganda