Uchunguzi umebaini kuwa vijana waliouawa Buruburu walikuwa wahalifu

  • | Citizen TV
    8,936 views

    Sasa inaibuka kuwa vijana wanne waliouawa kwa kupigwa risasi katika eneo la Buruburu jijini Nairobi wana rekodi za uhalifu jijini Nairobi na baadhi ya maeneo ya kaunti ya Kiambu. Wapelelezi wanaohusika na uchunguzi kuhusu ufyatuaji risasi mkesha wa krismasi wamefichulia runinga ya Citizen kuhusu matukio ya uhalifu ya genge lililojumuisha vijana hao ikiwemo wizi wa mabavu. Maelezo zaidi yanafichua kwamba genge hilo limekuwa likiendesha shughuli zake kwenye kundi la watu 5