'Ufuta nimevuna kwa wingi ila sasa kwenye soko, bei imeporomoka mno'

  • | BBC Swahili
    Shughuli za kiuchumi zinaendelea kama kawaida nchini Tanzania. Lakini kwa wafanyabiashara ya mazao ya kilimo ambayo wanategemea kuuza mazao ya nje ya nchi, yenyewe bado inachechemea. Kutokana na kufungwa mipaka na masoko ya kimataifa, wakulima wa ufuta kusini mwa Tanzania sasa wanalazimika kuuza kilo moja ya ufuta kwa kama Dola senti 56 tu - takribani nusu ya bei waliyoiuza ufuta msimu uliopita ambayo ilikuwa zaidi ya dola moja. Mwandishi wetu Sammy Awami alikwenda Lindi, Kusini mwa Tanzania kujionea hali ilivyo.