Ugonjwa wa akili umetajwa kuongezeka Kitui

  • | Citizen TV
    212 views

    Ugonjwa wa akili umetajwa kuongezeka mara dufu mjini Kitui katika siku za hivi karibuni. Akizungumza wakati wa siku ya matembezi ya kutoa hamasa kuhusu afya ya akili, mtaalamu wa akili katika hospitali ya rufaa ya Kitui Dkt Priscilla Makau alisema kwamba idadi ya walioathirika inaongezeka Kwa viwango vya kutisha. Dkt Makau alisema kwamba idadi hii inaweza kuongezeka zaidi iwapo walio na matatizo ya akili watakosa kuzuru hospitali ili kukaguliwa na wataalamu.