Uhaba wa samaki watia kiwewe wavuvi katika kaunti ya Kilifi

  • | Citizen TV
    568 views

    Uhaba mkubwa wa samaki umeanza kushuhudiwa katika kaunti ya kilifi jambo ambalo liwametia wasiwasi wavuvi wa eneo hilo wakati huu ambapo wakenya wengi Wanakumbwa na hali ngumu ya uchumi. Wavuvi hao wanadai kuwa hali hii inachangiwa na meli ambazo zinafanya uvuvi baharini. Wachuuzi wa samaki pia hawajasazwa na uhaba huo wa samaki kwani tayari wengi wamekua wakirudi mkono mtupu.