- 723 viewsShughuli ya kuchukua sampuli za msimbojeni yaani DNA za kusaidia kutambua miili ya wanafunzi walioangamia katika mkasa wa moto katika shule ya wasichana ya Utumishi eneo la Giligil imeanzishwa hii Leo. Hata hivyo, baadhi ya wazazi wameghadhabishwa na mwendo wa kinyonga wa shughuli hiyo na ukosefu wa mpangilio mwafaka wa kuwapasha habari.